Numbers 26:63-65

63 aHawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko. 64 bHakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Musa na kuhani Haruni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai. 65 cKwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.
Copyright information for SwhKC